KWA NINI KUFANYA TAFAKURI? (S.O.AP)

Ni kitu kimoja tu kurahisisha kusoma maandiko, ila ukiangalia kwa umakini, ukijifunza kwenda taratibu ili kusoma KWELI, ghafla maneno yaanaanza kujitokeza kwenye ukurasa. Kwa kufanya tafakuri ya mistari yako ya Biblia unaweza kuchimba chini zaidi katika maandiko na kuona zaidi kama ungesoma kawaida tu mistari na baadae kuendelea na ratiba zako.

Hebu nikutie moyo kutumia muda wa kutosha kufanya tafakuri (S.O.A.P) za mistari ya kila siku na kujionea mwenyewe vile unapata kila siku katika kusoma kwako kila siku….utashangaa.

JE, S.O.AP AU TAFAKURI MAANA YAKE NINI?

S – Inasimama kwa Maandiko-Unaandika kabisa neno la siku hiyo…utashangaa kile Mungu atakufunulia kwa kuchukua muda wako kwenda taratibu na kuandika unachokisoma!

O – Hii inasimama kwa Uchunguzi-unaona nini au umechunguza nini kwenye ile mistari ya Biblia uliyosoma? Anaandikiwa nani? Je, kuna maneno yamerudiwa mara kadhaa kwenye hiyo mistari? Ni maneno yapi yaliyokuvutia?

A – Hii inasimamia kuweka katika matendo au kulinganisha kinachosemwa kwenye mistari ya Biblia uliyoisoma na hali ya sasa. Hapa ndo pale tunaposema, neno la Mungu kuwa binafsi, Mungu anasema nini na mimi leo? Je ninawezaje kuweka katika matendo hiki nilichokisoma leo katika maisha yangu binafsi? Ni mabadiliko gani napaswa kufanya katika maisha yangu kutokana na kile nilichokisoma kwenye neno la leo? Je kuna hatua yoyote napaswa kuchukua?

P – Na mwisho kabisa hii P inasimamia Maombi.Omba neno la Mungu kulirudisha kwake, kama amekufunulia chochote kwa wakati huu kupitia neno lake, kiombee. Tubu kama amekufunulia dhambi ambayo ipo katika maisha yako.Kusoma neno la Mungu namna hii linawekza kukuchukua muda mfupi au mrefu kidogo kutokana na muda ulionao.Kwa siku nyingine inaweza kukuchukua dakika 10 au 15, siku nyingine dakika nyingi zaidi ya hizo.

JE, NITAFANYAJE TAFAKURI (S.O.A.P)?

Huu ni mfano binafsi….

Wakolosai 1: 5-8

S– Kwa sababu ya tumaini mlilowekewa akiba Mbinguni; ambalo habari zake mlizisikia zamani kwa neno la kweli ya injili, iliyofika kwenu, kama ilivyo katika ulimwengu wote, na kuzaa matunda kwa kukua, kama inavyokua kwenu pia, tangu siku mliposikia mkaifahamu sana neema ya Mungu katika kweli; kama mlivyofundishwa na Epafra, mjoli wetu mpenzi, aliye mhudumu mwaminifu wa kristo kwa ajili yenu; naye alitueleza upendo wenu katika Roho.

O– (Mara kadhaa nimekuwa nikiorodhesha chunguzi zangu….. ninachokiona tu pale mwanzo ninapopitia mistari) 

  • Unapounganisha imani na upendo, unapata tumaini.
  • Tunapaswa kukumbuka kuwa tumaini letu liko mbinguni…bado halijaja.
  • Injili ni neno la kweli.
  •  Injili inaendelea kuzaa matunda na inakua kuanzia siku ya kwanza mpaka ya mwisho.
  • Inamchukua mtu mmoja kuibadili jamii nzima……….. Epafra.

A– Kitu kilichosimama kwangu leo, ni namna Mungu alivyomtumia mtu mmoja, Epafra kuubadili mji mzima!!! Nimekumbushwa kwamba tunaitwa tu kuwaambia wengine habari za Kristo…….ni kazi ya Mungu kuieneza injili….kuikuza na kuifanya izae matunda. Nimehisi mistari ya leo ni kama imesema moja kwa moja kwa huduma hii ya LGG…..“duniani kote injili hii inazaa matunda na yanakua, kama ilivyokuwa ikifanya katikati yenu tangu siku mlivyoisikia na kuielewa neema ya Kristo katika kweli yake.” Je si jambo la kufurahisha pale ambapo neno la Mungu linakuwa hai na kusema moja kwa moja mahali tulipo?!!!! Maombi yangu leo ni haya, wanawake wote walioshiriki katika somo hili la Biblia wataelewa neema ya Mungu na kuwa na kiu na neno lake.

P– Ee Bwana, tafadhali nisaidie kuwa Epafra…..kuwaambia wengine kuhusu wewe na kuacha matokeo katika mikono yako pendwa. Tafadhli nisaidie kuelewa na kukiishi kile nilichosoma leo katika maisha yangu binafsi, kwa kuwa kama wewe zaidi na zaidi kila siku na kila mara. Nisaidie kuishi maisha yanayokuzalia “matunda” ya imani na upendo ……nikiliitia tumaini langu mbinguni, na si hapa duniani.Nisaidie kukumbuka kuwa mambo mazuri zaidi bado yanakuja!  

Mambo muhimu katika mbinu hii ya (S.O.A.P)/Tafakuri ni mwingiliano wako na neno la Mungu na kuliweka katika matendo neno hilo katika maisha yako.

RASLIMALI ZA MBINU HII YA TAFAKURI

Masomo yote ya huduma hii ya Mpende Mungu Sana yameundwa kwa kutumia mbinu ya tafakuri. Masomo yetu yatakutia moyo kuingiliana au kujichanganya na kukua kwa kina katika neno la ajabu la Mungu!

Asilimia mia moja 100% ya manunuzi yako inaenda kwenye
huduma yetu kutusaidia kutoa neno la Mungu kwa wanawake duniani kote katika lugha zao. Mpaka sasa tunakarimani katika lugha 40+ na tunataka tuendelee kukua.

Ununuzi wako unasaidia huduma yetu kukua!