Kauli ya Imani

Utume wetu wa kuwasaidia wanawake kumpenda Mungu sana kwa amaisha yao, imetokana na imani zetu kuhusu Mungu na jinsi ambavyo amejidhihirisha kwetu kupitia Biblia.

Huu hapa ni muhitasari mfupi wa kile tunachokiamini kuwa kweli:

Imani ya Nikea

Tunaamini katika Mungu mmoja, baba, Muumba wa mbingu na nchi, na vyote vinavyoonekana na visivyoonekana.

Tunaamini katika Bwana mmoja, Yesu Kristo, Mwana wa pekee wa Mungu aliyezaliwa milele na Baba, Mungu kutoka kwa Mungu, Nuru kutoka kwa Nuru, Mungu wa kweli kutoka kwa Mungu wa kweli, aliyezaliwa na hakuumbwa mmoja wa kuwa na Baba. Katika yeye vyote vilitengenezwa. 

Kwetu sisi wanadamu na kwa wokovu wetu alikuja chini kutokea mbinguni:
kwa uweza wa Roho Mtakatifu akawa mwili kutoka kwa Bikra Maria, na akafanyika mwanadamu.

Kwa ajili yetu alisulubishwa na Pontio Pilato; alikufa na alizikwa. Siku ya tatu alifufuka tena kama maandiko yanavyosema; alipaa kwenda  mbinguni na ameketi mkono wa kuume wa Mungu Baba mwenyezi na kutoka huko atakuja katika utukufu wake kuwahukumu walio hai na wafu na ufalme wake hautakuwa na mwisho.

Tunamwamini Roho Mtakatifu, Bwana na mtoa Uzima, anayeendelea kutoka kwa Baba na Mwana anaabudiwa na kutukuzwa.Amesema kupitia Manabii. 

Tunaamini katika kanisa moja katoliki* na mitume.

Tunakubali ubatizo mmoja kwa ondoleo la dhambi. 

Tunatazamia kufufuliwa kwa wafu, na uzima wa ulimwengu ujao. Amina. 

*Matumizi ya neno “katoliki” katika Imani hii ya Mitume haihusiani kabisa na kanisa Romani Katoliki, ila neno, katoliki lina maana ya jumla/ujumla. Ukiri wa imani katika “katoliki takatifu na kanisa la mitume” maana yake tunaamini kuna mwili mmoja wa waamini ambao katika Yesu Kristo pekee ndiyo msingi na kupitia yeye pekee tunaweza kuwa na umoja na waamini wengine.

Muhtasari wa Imani

Biblia ni neno la Mungu lisiloweza kushindwa.Mungu ni utatu katika mmoja: Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.

Uungu wa Yesu , kuzaliwa na bikira, ubinadamu usio na dhambi, upatanisho wa kifo msalabani, ufufuo wa mwili na kupaa mbinguni. 

Wote tumetenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu. 

Wokovu ni kwa neema tu kuwa na imani pekee katika Kristo.

Roho Mtakatifu hukaa ndani ya waamini na kuwawezesha kuishi maisha ya Kikristo.

Kristo atarudi kuhumu walio hai na wafu.

Kufufuliwa kwa mwili: uzima wa milele kwa waamini wote wa kweli mbinguni na adhabu ya milele kwa wasioamini wote kuzimu. 

Kanisa limetengenezwa na waamini wa kweli kutoka makabira yote, lugha zote na mataifa yote.

Waamini wanaamriwa kuwaambia wengine habari njema za Injili.