Tungependa kukualika kwenda zaidi ya masomo ya Biblia na uwe sehemu ya huduma hii ya Mpende Mungu Sana/LGG kwa kutuunga mkono, kwa kununua masomo au kupitia sadaka, au kwa kutumika pamoja nasi.
Wanawake ambao wanaweza kutafsiri maandishi kutoka Kiingereza hadi kwenda Kiswahili. Tunahitaji ujuzi mkubwa wa lugha zote mbili. (Uzoefu wa kitaaluma unapewa kipau mbele.)
Katika LGG, vifaa vyote tunavyoandika au kutafsiri vinapitiwa na kuhaririwa kabla ya kuchapishwa. Tunahitaji wahariri wa nakala kutusaidia katika kazi hii.
Mahitaji ya kuwa mhariri ni ujuzi mkubwa wa lugha ya Kiswahili katika msamiati, sarufi, maneno yaliyoandikwa, na maarifa ya kibiblia.
Wanawake ambao wanajua jinsi ya kutumia (au wako tayari kujifunza jinsi ya kutumia) Canva, Photoshop au mhariri yeyote wa picha mtandaoni ili kufanya picha zinazohitajika kwa kila funzo la Biblia.
Je, una shauku ya kuwasaidia wanawake wengine kukua katika maisha yao ya kiroho?Tunataka kufanya nyenzo zetu na mafunzo ya uongozi yapatikane kwako ili uweze kuunda kikundi chako cha mafunzo ya LGG na kuwasaidia wengine kukua katika Bwana.
Sote tunahitaji kutiwa moyo. Kwa sasa tunatafuta wanawake ambao wana kipawa cha kutia moyo na shahuku kusaidia kujenga dada zao katika Kristo. Kujitolea katika eneo hili kunaweza kujumuisha kutumika kwa kujibu maoni, kuomba kwa wengine, kutoa links na mafaili, kukusanya jumbe zilizoandokwa na watu…
Tunajua unataka kuleta mabadiliko! Jiunge na huduma hii ya Mpende Mungu Sana, juu ya utume wa kupambana na kutojua kusoma na kuandika kibiblia ulimwenguni kote, na kutoa rasilimali za kujifunza Biblia katika lugha nyingi kadri tuwezavyo.
Kama shirika lisilo la faida, Huduma hii ya Mpende Mungu Sana kwa sababu ya ukarimu wa wanawake kama wewe ambao ulichagua kuwekeza katika mambo muhimu kweli. Kila mchango huleta mabadiliko milele!